GET /api/v0.1/hansard/entries/1565209/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565209,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565209/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kusema machache kuhusu mimba za mapema za watoto wetu. Mahali ninapotoka, Tana River, shida hii bado ipo na inazidishwa na tabia ya kuoa mapema. Nachukua nafasi hii kwanza kushukuru korti zetu za upande wa Tana River ambazo zimewafunga watu waliopatikana na hatia hii. Watoto wanaojihusisha na kitendo hiki wameanza kufuatiliwa, lakini mambo haya yameendelea kwa muda mrefu. Kwanza nawashukuru machifu na makamishna wasaidizi wa kaunti. Licha ya kufungwa kwa watu wanaohusika na kitendo hiki, machifu na makamishna wasaidizi wa kaunti wamesaidia kuelimisha wananchi kila sehemu. Tunashukuru sana kwa kazi wanayoiendeleza."
}