GET /api/v0.1/hansard/entries/1565212/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1565212,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565212/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo la pili na la mwisho kuhusu hizi mimba za mapema, naomba wazazi wawe na muda wa kukaa na watoto wetu. Wakati wanapotoka asubuhi kuenda shambani, kuuza sokoni, kuenda shuleni au kuchunga mbuzi na ng’ombe, wanaporudi jioni, tuchukue nafasi kukaa na watoto wetu. Dunia imechafuka sehemu nyingi ikiwemo kwa mitandao, mazungumzo na hata sehemu ambazo watu wanakunywa pombe. Kwa hivyo, kama wazazi, tuchukue jukumu la kuongea na watoto wetu. Kwa kiingereza tunasema, “ push back”. Kama ilivyosemekana hapa, mimi ni mzazi wa wasichana. Nilidhani kwamba ili watu wafahamiane wanaenda kuongea huku wakinywa chai, kisha baadaye wanaenda kwa mkahawa ama kwa mbuga ya wanyama ama kununua njugu na kukaa chini ya miti. Nilikuwa sijui kwamba siku hizi mambo ni tofauti. Wasichana wangu wamenieleza yale mambo yanayoendelea duniani. Nimeshtuka kujua kwamba siku hizi kila kitu kinafanywa kwa mtandao na sio kama zamani. Wasichana wangu wananieleza ya kwamba hawawezi kuenda kufahamiana na mtu huku wakila njugu. Mambo yamebadilika na sio kama zamani tena. Kwa hivyo, ni lazima tukae na tuwaongeleshe hawa watoto wetu. Hii ni kama vita kwa sababu usipowaongelesha, ukweli wa watoto wako utakuwa ni ukweli wa wale watoto ambao wako na tabia mbaya. Ukweli wa watoto wako itakuwa zile video chafu ambazo wanaangalia katika internet na zile stori wanaambiwa na watu wengine. Lazima tuchukue nafasi ya kupinga kabisa haya mambo na kuwafundisha maadili na dini. Isikuwe kwamba tunawangojea watu wa kanisa ama watu wa madrasa wawafunze dini. Sisi wenyewe kule nyumbani, lazima tukae na kuomba na watoto wetu; tuongee nao na tuwafunze ili mambo haya ya mimba zisizo takikana yapungue. Bw. Spika wa Muda, kati ya mambo mengi ambayo lazima tufanye sisi kama Wakenya, lazima tuchukue majukumu yetu kama wazazi ili kupigana na hizi mimba za mapema. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}