GET /api/v0.1/hansard/entries/1565213/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565213,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565213/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Murgor",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hii. Mimba za mapema ni kitu ambacho kimeshika mwendo sana siku hizi. Ninaunga mkono yale wenzangu wamesema kwamba umaskini umezidi na ndipo watoto wanajipata tu wanaongozwa kufanya haya maneno kupitia njia ambazo ni rahisi kama kununuliwa switi na biskuti. Vitu kama hivi vinafanya watoto wachukuliwe na watu walio na nia mbaya. Njia ambayo imekuwa rahisi sana ni watu wa pikipiki hasa ambao wanabeba watoto wetu na kuwapeleka shuleni, sokoni ama kuenda pahali ambapo wanataka kuenda. Kuna watu fulani ambao huwa wanajifanya wanawasaidia na hata saa zingine wanawabeba bure bila malipo. Kwa njia hii, wanaweza kulala nao na kuwapachika mimba. Utapata ya kwamba kule nyumbani baba na mama siku hizi hawajali kuketi na watoto wao na kuwaongelesha. Zamani wamama walikuwa wanaongelesha hasa wasichana wale ambao wameanza kupata hedhi. Wamama walikuwa wanajua ya kwamba bila shaka wataweza kupata mimba wakati wowote. Kwa hivyo, walikuwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}