GET /api/v0.1/hansard/entries/1565214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1565214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565214/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Murgor",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wanawakaribia kabisa, kuongea nao na kuweka maneno wazi, ili msichana ajue ya kwamba akilala na mwanaume, mimba inaweza kupatikana wakati wowote. Siku hizi wamama wameachia walimu wawe ndio wanakaribia watoto na labda wanawaachia watu wa kanisa ama madrasa waongeleshe watoto. Hata hivyo, hao pia saa zingine wengine huko wanakuwa nyangau ama wale ambao wataweza kutumia hao watoto vibaya. Kwa hivyo, kila pahali sasa ni hatari kwa mtoto msichana na mvulana pia. Hii ni kwa sababu watoto wavulana pia wameingia katika hali hiyo ya kutumiwa vibaya na watu walio na nia mbaya. Ili tuweze kukabiliana na hali ambayo tukonayo sasa ni kuongea na watoto kwa njia ambayo ni wazi. Haswa, baba na mama wenyewe wanastahili waongee kwanza na wajadili juu ya watoto wao na mienendo ya kila mtoto vile anaendelea, ili waweze kuwasaidia wasiweze kutumiwa vibaya na wajikute wako mimba. Mtoto msichana akisha pata mimba ni kama mwisho wa barabara ya maisha yake ya kesho. Hata ingawa tunapiga piga kiraka kidogo, tunasema aache mtoto pahali na arejee shuleni, lakini huyo ni mtu ambaye tayari ameumia na hali yake vile alikuwa huru na aliota ndoto zake za baadaye yanaanza kudimimia na kuwa mtu ambaye amenusirika hali ambayo haiwezi kumuendeleza katika maisha yake. Pia, hii tabia ya wazazi haswa wazee kuingia sana katika mvinyo, inawaweka katika hali ya kutojali. Wao sasa hawaoni watoto wao wanaelekea aje kwa sababu wanaingia nyumbani wakati ambao watoto wamelala. Kwa hivyo, inafaa wazazi wajirekebishe kabisa ili waweze kustahimili yale ambayo yanawakumba watoto wao kwa wakati wa sasa. Asante."
}