GET /api/v0.1/hansard/entries/1565383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1565383,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565383/?format=api",
    "text_counter": 68,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundig",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Naunga mkono Hoja hii ambayo inahusika na mambo ya kilimo cha kahawa. Siku hizi tuna uwezo wa kusherehekea mambo ya kilimo kwa sababu yako katika serikali gatuzi. Pia tunashukuru Serikali ya Kenya Kwanza kwa sababu imekuwa ikiangalia vile mkulima ataweza kufaidika. Tumegundua ya kwamba wakati Serikali hii iliingia mamlakani, watu wengi walikuwa wameanza kukata miti ya kahawa mashinani na wakaanza kupanda mimea mingi. Hata hivyo, wakati huu tunasherehekea. Katika kaunti zingine utakuta viwanda vingine vya kahawa vinauza kahawa kwa Shilingi 150 kwa kilo zingine shilingi 130 kwa kilo kutoka Shilingi 40 kwa kilo. Kwa hivyo, ninaunga mkono tuweze kuangalia vile mkulima ataweza kufaidika. Tunakumbuka wazazi wetu wazamani walikuwa wanafunzwa kuhusu kilimo cha kahawa. Zile kaunti zilizokuwa zinapanda kahawa zilikuwa zinasherehekea sana. Familia zao zilikuwa zinaendelea vizuri. Hata hivyo, kwa miaka mingi iliyopita, mambo iligeuka lakini sasa tunasherehekea kwa sababu Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto, alikuja akawaunganisha watu wote pamoja. Alisema mambo ya cartels iondolewe na akaondoa ushuru kwa mambo mengi. Sasa tunajivunia. Bw. Spika, mimi ninaunga mkono jambo hili. Tukiendelea vile tunaendelea, mkulima wa kahawa katika Kenya nzima atakuwa anajivunia. Hii kwa sabau bei ya kahawa itafika Shilingi 200. Sio kahawa pekee yake, kuna mambo mengi tunastahili tuyaunge mkono. Kuna mambo ya majani, macadamia, maembe, avocados na pia miraa au ‘ muguka.’ Katika nchi ya Kenya, mambo ya kazi imekosekana. Wazazi wengi pia wamekosa pesa ya kupeleka watoto wao shule. Hata wale watoto wetu ambao wamesoma vizuri na wakasoma katika shule hata ya juu na kuenda vyuo vikuu vya degree, imekuwa hakuna kazi. Bw. Spika, tukiendelea hivi, utakuta katika kaunti 47, mambo ya kilimo itaweza kupewa kipaa umbele. Mambo ya kilimo iko katika serikali za kaunti. Kwa hivyo, tungeomba serikali gatuzi ziweze kuipa kilimo kipa umbele . Tumeona magavana na wafanyi kazi wengine hawasaidii katika mambo ya kilimo. Nikiongea juu ya mambo ya kahawa, wiki jana tulitembea kule Bungoma na Kisumu. Tuliona kuna watu wengine ambao wanauza kahawa kwa Shilingi 145 lakini katika kaunti zingine, kahawa ni Shilingi 35. Katika kaunti zingine maziwa inauzwa kwa Shilingi 52 ilhali kaunti zingine maziwa ni Shilingi 44. Haya ni mambo ya kuhuzunisha kwa sababu kuna matapeli wengi. Kuna watu wanaosimamia mambo ya vyama. Ningeomba mambo mengi yaweze kulainishwa. Tukifanya hivyo, mkulima wa kahawa na wakulima wa mazo mengine watafaidika vizuri. Bw. Spika, naunga mkono nikiwa Seneta wa Embu Kaunti. Ninafurahia katika Embu Kaunti mambo ya kahawa yamepewa kipau umbele. Mwisho ni kuomba serikali za kaunti na wizara husika na ukulima na mifugo iweze kupelekwa mashinani ili tuweze kujivunia katika mambo ya kilimo. Asante, Bw. Spika."
}