GET /api/v0.1/hansard/entries/1565502/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565502,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565502/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Watu wamesahau ya kwamba sisi Maseneta tuko hapa kutetea devolution. Serikali za kaunti zilipatiwa department kumi. Mara nyingi kumekuwa na shida kwa sababu pesa ambazo tumepewa ni kidogo sana na hata department zingine hazipati pesa. Pesa nyingi zimekuwa zikienda upande wa hospitali, kilimo na barabara. Hata hivyo, unapata kwamba hizo pesa hazitoshi kushughulikia mambo mengine kama mifugo. Tumeshuhudia magavana wengi wakipata shida kwa sababu wakati walipoingia ofisi walipata kuna pending bills na wage bills kubwa. Mfano ni Kaunti ya Embu. Hapo awali hapakuwa na usawa katika ugavi wa pesa kwenye makaunti. Tuliona kwamba kaunti zile ambazo zilikuwa hazijiwezi zilikuwa zinapatiwa pesa nyingi na zile kaunti ambazo zilikuwa na uwezo mkubwa zilikuwa zinapatiwa pesa kidogo. Ikafika wakati wakufanya audit ili kuona kama hizo pesa zimesaidia hizo kaunti kujimudu na zilitumika kwa njia inayofaa. Mimi ninaunga mkono counties ziweze kupewa Ksh465 bilioni ili ziweze kufanya kazi vile inatakikana. Kila wakati sisi tumeona CHPs wakija hapa kwa gate ya Bunge, wakiandamana. Hii ni aibu sana. Tungependa MPs wa Bunge la Taifa, Serikali Kuu na Treasury wajuwe kwamba Seneti inataka CHPs, madaktari na watu wengine wapatiwe pesa. Tumeona wafanyi kazi wa county government wakichelewa kupata mishahara yao na pia tunaona vile hali ya uchumi inaendelea kuwa . Pay slips nyingi zimekuwa na shida kwa sababu mambo ya ushuru wa nyumba na hata SHA zimeenda juu. Kama county governments watapata pesa, wataweza kuongezea wale wafanyikazi ili wawache kulia. Magavana wengi wako na shida kwa sababu tunaona wakati mvua inanyesha hawapati pesa za kutengeneza barabara. Kwa sasa, SHA inafanya kazi lakini magavana wanalia kwamba hakuna pesa za kununua dawa katika mahospitali. Kwa hivyo, mambo mengi yanafaa kuangaliwa. Pia mambo ya kilimo inafaa kuangaliwa. Wakati tulikuja hapa Seneti, tulipitisha tuwe CHPs na pia kuwe na agricultural extension officers. Lakini kutoka wakati huo, wengine wajawahi kupata pesa. Kama counties zitaweza kupata pesa kwa njia ambayo inafaa, hawa watu wote wataweza kulipwa mishahara yao. Mimi nikiwa Seneta wa Kaunti ya Embu, ninasema counties ziweze kupatiwa pesa. Tumesikia MPs wakisema ya kwamba counties hazitumii pesa vile inavyotakikana. Mimi ninakataa kwa sababu, kazi yao ni kupitisha pesa ikuje Seneti, ili Seneti iweze kufanya ugavi kulingana vile inafaa kuwa ndio kaunti zote ziweze kupata pesa sawa. Kazi ya Seneti ni oversight na kuangalia vile pesa inafanya kazi; hiyo sio kazi ya MPs. Tutapitisha budget ili counties zipate pesa. Pia mambo ya the National Treasury, ninakumbuka wiki jana, Waziri wa Fedha alitakikana kuja Seneti ili kujibu maswali lakini hakuja. Kwa hivyo, mambo ya Treasury inafaa kuangaliwa ili tuone kama kuna shida ndio Waziri aweze kupatia counties zetu pesa na wananchi waweze kufaidika. Wakati huu tumeona counties nyingi zimeweza kufanya kazi na pia magavana wanafanya kazi. Kusema ukweli magavana katika kaunti nyingi wanateseka sana. Wafanyikazi wanachelewa kupata mishahara na watu wengi hawapati pesa vile inafaa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}