GET /api/v0.1/hansard/entries/1565503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1565503,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565503/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ninakumbuka katika Kaunti ya Embu kulikuwa na shida wakati pesa iliyotolewa kwa ajili ya kununua chakula ilichelewa. Na wakati pesa ilikuja, gavana aliweza kununua mahindi akiwa amechelewa na utapata mpaka sasa huenda pesa za fertilizer hazijapeanwa ili gavana apelekee wakulima. Wakati mwingine magavana wako na ujuzi wa kufanyia wananchi kazi lakini unapata pesa zinachelewa kutoka. Kwa hivyo, wakati mwingine sio magavana ndio wako na shida; shida inatokana na Bunge ama National Treasury ambapo pesa zinatoka. Mwaka jana pesa hazikutosha. Tungependa wale Maseneta professionals ambao watachaguliwa kuenda kufanya mediation na Bunge la Kitaifa, waweze kuangalia kwamba ile pesa isipunguzwe na hata kama itapunguzwa, iende chini kidogo ndio tuweze kusaidia ugatuzi na economy za kaunti zetu ziweze kuendelea vizuri. Tumeona kwamba walipopata pesa kidogo, wameweza kuendeleza mambo ya kilimo. Wameendeleza ukulima wa majani chai, kahawa macadamia, maembe na mimea mingine. Magavana wanataka kuwe na value addition na Serikali ya Kenya Kwanza inaunga mkono. Tunataka miraa na muguka ifanyiwe value addition ndio watu waweze kuisimamisha ili katika miaka ijayo serikali kuu na serikali za ugatuzi ziweze kuendelea vizuri na economy ya kaunti zote iweze kuendelea."
}