GET /api/v0.1/hansard/entries/1565745/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1565745,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565745/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia kauli hizi. Ni vizuri ijulikane ya kwamba watu wanaofanya biashara za rejareja wana haki, kwa sababu wanachangia kwa maendeleo ya nchi. Ikumbukwe sisi tukifanya siasa tulisema ya kwamba wale walala hoi, wanapaswa kuangaliwa. Haitakubalika na ni jambo la kuvunja moyo sana, ikiwa wale wanafanya biashara za rejareja hawapewi fursa, wanahangaishwa na kusumbuliwa. Hawawezi wakasimama mahali popote katika Jiji hili au sehemu zozote katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, sisi sote tuna haki ya kufanya biashara mahali popote. Kamati ambayo itashugulikia jambo hili, ijue watu wote wanafaa kupewa uhuru wa kufanya biashara. Iwe biashara kubwa, rejareja au yeyote ile, ikiwa mtu amefuata"
}