GET /api/v0.1/hansard/entries/1565756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565756,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565756/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kama wenzangu wametangulia kusema, wale wametwikwa jukumu la kulinda misitu, wamekuwa wakilala katika kazi zao. Na wakati ambapo wananchi au mashirika tofauti wanapoleta mambo haya kwa mwanga, hapo ndipo wale walio na jukumu hili la kulinda misitu wanakuja na kutupea vijisababu vya kusema ni kwa nini kumetokea mambo kama yale. Kama mwenzangu moja alivyosema, juzi pale Karura walipokuwa wakikata misitu, walisema walikuwa wanaondoa ile miti ya zamani ili kupanda miti ya kisasa. Lakini, walikuwa wanakata miti yote. Ikiwa walikuwa wanaondoa miti ya zamani na kuleta miti ya kisasa, wangekata michache na kuacha mingine. Wanapokata miti kwa kijumla, tunashuku kuna watu wanaotaka kufanya majengo ndani ya misitu. Bw. Spika, kulingana na Katiba, ni lazima kabla ya kukata miti ndani ya misitu, umma uulizwe maoni yao na wayatoe. Ni lazima Kamati itakayochunguza suala hili ituambie, je, umma ulihusishwa? Je, umma ulipohusishwa, waliamua aje? Je, walipitisha kwamba hoteli ijengwe mle ndani ya msitu na hoteli ile inajengewa nani? Ni nani mwenye hiyo hoteli pia? Kilicho muhimu sana ni kujua ni nani anayejenga hoteli ndani ya msitu. Ninaamini anayejenga ndani ya msitu ni lazima ni mtu aliye na ushawishi mkubwa ndani ya Serikali. Ni lazima tujue ni nani. La mwanzo kwangu ni, ni lazima tujue ni nani ili tujue huyu anayejenga bila kuhusisha umma au bila kuulizwa na maofisa waliopatiwa jukumu la kulinda misitu. Bw. Spika, ni lazima pia tujiulize, je, ni miti iliyokatwa pale ama palikuwa ni mahala hapana miti? Je, kuanzia sasa kwenda mbele, tutahakikishiwa na nani kwamba misitu yetu iko salama? Tutahakikishiwa na nani kwamba misitu yetu haitaendelea kukatwa? Hili ni jambo ambalo Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili inafaa iangalie kwa makini sana. Ninaamini Mwenyekiti wangu, Seneta wa Mombasa, Seneta Faki, ameyasikia haya na atayapatia kipau mbele."
}