GET /api/v0.1/hansard/entries/1565774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565774,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565774/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Mswada wa Ugavi wa Fedha wa mwaka 2025/2026. Mswada huu ni muhimu katika nchi yetu kwa sababu ndio kinara ya miswada yote ambayo inahusiana na masuala ya fedha. Baada ya hii, tutakuwa na Mswada wa County Allocation of Revenue Bill (CARA) ambayo inagawanya fedha kati ya kaunti zetu. Baada ya hiyo, tutakuwa na Appropriations Bill ambayo inatoa pesa kutoka kwa hazina kuu."
}