GET /api/v0.1/hansard/entries/1565779/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565779,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565779/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba nisikizwe kwa makini. Kuna Seneta hapa mbele yangu ambaye anatoka Kaunti ya Migori--- Mwaka huu, tumeona ya kwamba Serikali imejizatiti na kupendekeza ya kwamba Shilingi bilioni 405 iende katika kaunti zetu. Tutakumbuka ya kwamba mwaka jana, Bunge la Seneti lilipitisha ya kwamba Shilingi bilioni 415 ziende katika kaunti zetu. Tulipoenda katika maelewano, tulikubaliana na Mswada wa kupeleka Shilingi bilioni 335 katika kaunti zetu kwa mwaka wa 2024/2025. Kwa hivyo, ni makosa kwa Serikali Kuu kupendekeza pesa ambazo mwaka jana, sisi kama Bunge la Seneti, tulisema hazitoshi kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, ukiangalia asilimia ya fedha ambazo zinakuja katika kaunti zetu kutoka mwaka wa 2013 mpaka sasa, utaona ya kwamba hiyo asilimia imekuwa ikipungua. Ijapokuwa tunaona ya kwamba pesa zinaongezeka, ukweli ni kwamba asilimia ya pesa inazidi kupungua. Kwa sasa, hiyo pesa ni chini ya asilimia 15 ya pesa ambazo zilikuwa zinaletwa katika kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, changamoto ambazo Serikali kuu inapata kukusanya kodi katika nchi yetu ni zile zinazokumba kaunti zetu. Kwa mfano, kama ni hali ngumu ya biashara, nchi nzima inapitia hali hiyo. Kwa hiyo, yale yanayoathiri kaunti, yanaathiri Serikali kuu vile vile. Kwa mfano, magari yanayosafiri katika kaunti yananunua mafuta kwa bei ile inayouziwa Serikali kuu. Haiwezekani Serikali kuu ijiongezee hela katika mgao, ilhali serikali za kaunti zinaendelea kupata shida."
}