GET /api/v0.1/hansard/entries/1565782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1565782,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565782/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tumegundua pia kwamba changamoto moja inayokuba kaunti zetu ni ucheleweshaji wa mgao unaotolewa kwa kaunti zetu. Kwa mfano, malipo ya mwisho kufanywa ni ya Mwezi wa Tatu. Yaani wako nyuma na karibu miezi miwili. Changamoto nyingine inayokumba serikali za kaunti ni kwamba haziwezi kulipa kodi ya mapato yaani, “pay as you earn”, na kodi zingine zinazokusanywa na serikali za kaunti ili kupeleka katika hazina kuu. Kwa hiyo, iwapo hizi pesa zitaendelea kuchelewa, utenda kazi kwa kaunti zetu utazorota na ukusanyaji wa fedha kwa Serikali kuu utadorora. Hii ni kwa sababu zile pesa zinazoenda katika kaunti ndizo zinazolipa kodi kwa wale wafanyakazi wa kaunti na kuwapa fursa ya kulipa kodi hii. Katika Mswada huu, tumeona kwamba Serikali kuu imetoa Hazina ya Usawa. Ijapokuwa hazina hii ilianzishwa mwaka wa 2012 baada ya kupitisha Katiba yetu, pesa hizi zimeendelea kukaa katika Serikali kuu. Hii ni kwa sababu kulikuwa hakuna sheria endelezi ya kutoa pesa hizi kutoka Serikali kuu hadi kaunti. Ilibidi Bunge la awamu ya 12 ipitishe sheria ili pesa zile zirudi kwa kaunti. Kwa hiyo, kuna malimbikizo ya madeni ya miaka mingi ambayo hayakuenda katika kaunti zile. Kuna pesa takribani Shilingi 2,736,739,351 ambazo Hazina ya Usawa inadai Serikali kuu. Pesa hii inasaidia kupunguza zile tofauti zilizopo kimaendeleo katika kaunti. Kwa mfano, kuna sehemu hazina maji safi au zahanati. Pesa hii ilinuiwa kufanya kazi hiyo. Iwapo pesa hizi zitaendelea kucheleweshwa ama kutopelekwa katika kaunti au Hazina ya Usawa, kazi zinazotarajiwa kufanywa katika maeneo yale ili yawe sawa na kaunti zingine zinaendelea kuchelewa. Hivyo basi, hakutakuwa na usawa ijapokuwa hazina hii ilibashiriwa kutumika kwa muda wa miaka 20. Kuna umuhimu wa Serikali kulipa yale malimbikizo ya madeni yaliopo ili hazina iweze kufanya kazi na watu waweze kupata maendeleo yaliyokusudiwa kutatuliwa na hazina hii. Jambo la mwisho, naunga mkono mapendekezo ya Kamati ya Fedha na Bajeti ya Bunge hili kwamba pesa zitakazogawiwa kaunti zetu ni Shilingi 465,001,459,673. Hii haimaanishi kwamba kaunti zetu zinapewa fedha kufanya ubadilifu. La hasha, hizi ni fedha zitakazowawezesha kusimamia bajeti zao kisasawa. Kwa mfano, kuna wahudumu wa afya ambao lazima watusalimie hapa Bunge kila wiki. Juzi kumetolewa agizo kwamba wengine wao wahamishwe kwa kaunti. Je, iwapo watahamishwa kuenda kwa kaunti na kaunti hazijapelekewa pesa, watalipwa na nini? Kuna huduma muhimu za afya ambazo wanapeana. Iwapo watakosa kulipwa mishahara, hali ya afya itadorora katika kaunti zetu. Wafanya kazi hawa wanafanya kazi muhimu sana ambayo haiwezi kudharauliwa. Bw. Naibu Spika, masuala ya SHA na kodi ya nyumba yameongeza mzigo katika kaunti zetu. Kwa hivyo, inapaswa mgao huu uongezeke ili kufidia yale mapengo ambayo yaliyosababishwa na pesa zinazokusudiwa kuenda kwa kaunti zetu. Hii haimaanishi kwamba hakuna ubatilifu katika kaunti zetu. Ukichunguza, utapata kuwa kila kaunti ina madhambi yake. Kwa mfano, Kaunti ya Mombasa ilipewa pesa takribani Shilingi milioni 100 za kujenga County Aggregated Industrial Park (CAIPs). Lakini ukienda katika viwanja vile utapata jiwe la msingi lililowekwa na Waziri"
}