GET /api/v0.1/hansard/entries/1565785/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565785,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565785/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wa zamani wa biashara, Mhe. Moses Kuria, mwaka jana mwanzoni. Hadi leo, hakuna jambo lolote linaloendelea katika maeneo yale. Tukiangalia masuala ya barabara, barabara nyingi katika Kaunti ya Mombasa hazipitiki kwa sababu ya mvua iliyonyesha. Barabara zote ikiwemo za kaunti pamoja na Serikali kuu ziko katika hali mbovu. Mji wa kitalii kama wa Mombasa haupaswi kuwa na barabara kama zile. Kaunti zetu zinapeana kipao mbele kwa mambo ambayo hayaendelezi kaunti zetu. Tukikirudi kwa masuala ya elimu, ijapokuwa kaunti zinafaa kushughulikia elimu ya chekechea na elimu ya kiufundi, Kaunti ya Mombasa ina taasisi mbili pekee za elimu ya kiufundi. Tulipozuru Kaunti ya Mombasa na Kamati ya Elimu ya Bunge hili, ilikuwa aibu kwetu. Kama watu wa Mombasa, tulishindwa kujieleza ni miradi gani tuliyoifanya kwa elimu ya kiufundi. Vituo vinavyotoa elimu ya kiufundi ni viwili pekee. Kimoja kipo maemeo ya Mtongwe, eneo Bunge la Likoni na kingine kipo maeneo ya Mwakirunge, eneo Bunge la Kisauni. Bw. Naibu Spika, kuna umuhimu wa Seneti kuchunguza kwa makini utendakazi wa kaunti zetu. Bila kufanya hivyo, tutakuwa tunapiga kelele na kukauka koo tukipendekeza pesa ziende katika kaunti, lakini hakuna maendeleo yoyote wananchi wetu wanapata. Mwisho, naunga mkono hukumu ya juzi iliyosema Bunge ipitie na kuidhinisha ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufikia tarehe 31 mwezi wa tatu. Hii ni kwa sababu itawezesha fedha ziweze kugawanywa kwa tarakimu sahihi. Katika Mswada huu, hesabu zilizotumika ni za mwaka 2020/2021 ambayo ni miaka mitano iliyopita. Kwa hivyo, Bunge likiweza kupitisha hesabu hizi kwa mapema zaidi, itakuwa ni vizuri zaidi kwa sababu pesa zitagawanywa kulingana na hesabu za sasa ambazo zinatumika katika Serikali kuu. Kwa hayo mengi, naunga mkono Mswada huu na vile vile naomba kwamba tuweze kupitisha hiyo Shilingi 465 bilioni. Asante, Naibu Spika."
}