GET /api/v0.1/hansard/entries/1565850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565850,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565850/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "May 21, 2025 SENATE DEBATES 38 Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir, for this opportunity. I plead to switch languages, so that I communicate to Kenyans. Asante kwa nafasi hii ili nichangie kuhusiana na mapendekezo ya fedha ambazo zapaswa kwenda kwa kaunti. Seneti imejieleza wazi kwamba tunahitaji Shilingi bilioni 460 ili kugharamia changamoto na hali ya maisha katika kaunti zetu na bajeti ambazo kaunti zimewasilisha katika mabunge yao. Wiki iliyopita vikundi vya Maseneta vimekuwa vikizuru pembe mbalimbali za nchi ya Kenya kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ugatuzi. Mimi ni mmoja wa Kamati ya Afya ambapo tulizuru kaunti ya Wajir, Marsabit na Mandera. Tuliyoyaona ni ya kusikitisha, kwamba baadhi ya kaunti ambazo tunazo hazina fedha za kutosha kununua mitambo ya kisasa ya matibabu na kuajiri matabibu ambao tumeona wakiandamana na wana ari ya kutoa huduma kwa Wakenya. Kamati ya Ardhi imezuru Kisii na Busia. Tunaona vile vile lazima sekta hiyo ipewe fedha za kutosha ili masuala ya ardhi katika kaunti yashughulikiwe. Iwapo hayo yote ni lazima yatekelezwe, ni lazima tuongeze kimo au fedha zinazoenda kwenye kaunti zetu. Bw. Naibu wa Spika, wiki iliyopita, nilikua na Kamati ya Ukulima, Uchumi Samawati na Ufugaji katika Kaunti ya Bungoma. Kulikuwa na ari au moyo kwa wakulima wa kahawa waweze kupata ardhi ya kuzindua taasisi ya utafiti au maabara ya kutafiti aina na ubora wa kahawa. Kama tunataka hivi vyote vitekelezwe, ni lazima bajeti zinazoenda katika kaunti zetu ziimarishwe. Kule kwetu, wakulima wa maziwa wanauza lita Shilingi 35, lakini kule maeneo mengine nchini, wanauza kwa Shilingi 50. Kile tunasema, ni lazima fedha ziongezwe katika makadirio ya bajeti ili magavana waweze kuajibika kwa fedha walizo nazo na Wakenya waandame fedha hizi kuhakikisha kwamba zinatekeleza majukumu yao. Kule Bungoma, Serikali imezindua baadhi ya soko pale Bukembe, ukija Misikhu, ukienda Webuye, Cheptonon na mji mkuu wa Bungoma. Serikali imeweka hizi soko kandarasi ili watu wachukue zabuni na kujenga. Lakini, itakuaje kwamba Serikali ya kitaifa inataka kufanya kazi ya kaunti ambazo zilipigiwa kura na magavana ambao wako na wajibu wa kujenga soko. Bw. Naibu wa Spika, tunashukuru Serikali kwa kuanzisha mchakato wa kujenga soko lakini tunaposonga mbele, bajeti ziwekwe kwenye kaunti zetu ili magavana na mawaziri wao wapange na viongozi wa wadi wadhibiti na kuchunga jinsi fedha hizi zinazotumika. Ndio sababu mimi nasema, Bunge la Taifa wana fedha wanataka zidhibitiwe katika mikoba yao lakini sisi kama Maseneta ni lazima tuhakikishe Wakenya ambao kila mara wanakamuliwa na ushuru, tuwafanyie kazi. Ukienda maeneo yaliyo na ukame, wana shida ya maji. Maji yamegatuliwa na ni lazima wawe na mitambo na mashine ya kuchimba maji ili kina mama wajinufaishe. Ukienda sekta ya vyuo anwai na shule za chekechea, utagundua baadhi ya maeneo ni vyumba peke yake vimejengwa na hakuna vifaa vya kutosha au vyakula virutubishi vya kuinua afya ya watoto. Pia hakuna walimu wa kutosha wa kufunza watoto hawa. Bw. Naibu wa Spika, itawezekanaje kaunti zitekeleze majukumu haya pasipo kua na pesa za kutosha ili kuhakikisha watoto wanapoenda shule, wanapata nafasi sawa na"
}