GET /api/v0.1/hansard/entries/1565856/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1565856,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565856/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika. Ninaheshimu uwezo na tajriba ya Seneta aliyeniuliza swali. Lakini, Wakenya wanaonitazama wanaelewa kwamba, kwa baadhi ya kaunti, watoto huona maziwa kwa vyombo vya habari. Watoto huona maziwa iwapo mwana wa mbuzi anapomnyonya mamake. Mambo ya chupa yasiwe ya muhimu sana. Cha muhimu ni mmoja anakunywa maziwa kwa chupa ya kawaida na mwingine anakunywa maziwa katika vijikombe vya mabati. Ninaomba nirejelee kwa Hoja. Ugatuzi uliletwa katika nchi ya Kenya kusawazisha maisha ya Wakenya na kuwaweka katika barasta iliyo sawa. Vyuo anwai na vyuo vya chekechea, ni lazima viwe na maabara, walimu wa kutosha na mashine na mitambo ya utafiti ya kutosha ili watoto wanapotoka Bungoma, Marsabit na Kisumu, wakikutana uwanja wa kutafuta kazi, wote wako sawa sababu ugatuzi uliwatendea wema wote, pasipo kunyimwa haki kikatiba. Ndio sababu ninaungana na Maseneta wengine na kusema kwamba, wakati umefika, magatuzi yapewe pesa za kutosha na tunapowapa pesa, tutawaandama kwa miradi ya maendeleo ili tuhakikishe fedha zinazoenda kwa miradi hii zinaenda sambamba na yale tunaona yakihadithiwa na macho mashinani. Nimegundua kwamba, ng’ombe wa kiuchumi ni miradi ghushi au miradi hewa. Yaani wanaweka mamilioni, lakini chini ya mamilioni haya, kuna wale wanakamulia chini kama wanakandarasi. Ni lazima Wakenya wawe macho kuhakikisha kwamba miradi inayotekelezwa, inaafiki matarajio yao na wanahusisha umma, kwa kimombo, public participation ili miradi iafiki matarajio ya wale wahusika ambao watanufaika na miradi hii. Bw. Naibu wa Spika, katika mapana na marefu, falsafa ya Serikali, ninaomba Jumba la Seneti lisimame wima, lisimame tisti, lisiumbishwe, lisipigiwe simu kutoka kwingine, tuamue jinsi tulivyoamua sasa na tutetee magatuzi yetu. Hizi pesa zinapoenda kule mashinani, vijana wengi mitandaoni hawana kazi. Ninaomba Seneti tuwachangamkie hao magavana. Kandarasi na pesa zinazopeanwa kule mashinani ni kwa baadhi ya makampuni zinazopewa ni makampuni yaliyoandaliwa kitaaluma ya watu fulani Nairobi, kunyima vijana wa mashinani kazi. Ni lazima tumulike hapo tujue. Asilimia 30 wanasema iwe ya watu wenyeji au 70 ya wenyeji. Lakini, ukimulika sana, baadhi ya wanakandarasi hawa si wenyeji na ni wale"
}