GET /api/v0.1/hansard/entries/1566350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1566350,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1566350/?format=api",
"text_counter": 103,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kutoa kauli yangu juu ya taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Abass, Seneta wa Gatuzi la Wajir. Mazingira ni kiungo muhimu cha maisha yetu. Kwa hivyo, ni makosa kwa serikali zetu za kaunti kuchafua mazingira ambapo binadamu wanaishi. Utupaji wa takataka ni donda sugu katika kaunti nyingi. Ijapokuwa kwa sasa kuna vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kutumika kubadilisha takataka kuwa umeme, makaa ama kwa matumizi mengine, kaunti zetu zimekuwa na tabia ya kutupa takataka bila uangalizi wowote."
}