GET /api/v0.1/hansard/entries/1566634/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1566634,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1566634/?format=api",
"text_counter": 51,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, naunga mkono Taarifa iliyoletwa na Kiranja wa Walio Wengi Bungeni kuhusu mfumo mpya wa afya wa SHA. Ni vizuri ijulikane ya kwamba, wakati tulipopata Katiba mpya, watu ambao walikuwa wakifanya kazi katika manispaa na gatuzi zingine, walijumuishwa katika gatuzi mpya. Vile vile, itakuwa bora zaidi wafanyakazi ambao walikuwa wa NHIF wajumuishwe katika mfumo mpya wa SHA, ndiposa hawa wafanyakazi wawe na uzoefu na walete utaratibu mpya katika sehemu ambazo hazifanyi vizuri. Kikatiba, itakuwa vibaya kuwadhulumu hawa wafanyakazi ambao wamefanya kazi na mfumo wa NHIF. Kisheria, wanapaswa kujumuishwa na kuendelea na kazi kwa sababu wamekuwa wakitegemea ile kazi na kuifanya kwa uzuri. Ni kwa sababu tu mambo yamebadilika na kumeletwa mfumo mpya. Ni vizuri wakumbukwe na wajumuishwe kwa sababu wana familia. Maisha yao yanapaswa kuendelea mbele na sisi tukiwa wawakilishi wao, na kitengo cha afya kikiwa kimepelekwa katika gatuzi zetu, tunapaswa kuifuatilia kuona kwamba inafanya kazi. Itafanya tu kazi ikiwa kuna vifaa na vile vile wafanyakazi. Kwa hivyo, wafanyakazi ambao wana mazoea na wamebobea katika ile kazi ni wale waliokuwa wa NHIF. Kwa hivyo, nakubaliana na hii Taarifa iliyoletwa na Sen. (Dr.) Boni ya kuweza kuwajumuisha wafanyakazi hao ili waweze kuendelea na kazi ambayo wamekuwa wakifanya. Bw. Spika, nashukuru kwa kunipa fursa hii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}