GET /api/v0.1/hansard/entries/1566645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1566645,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1566645/?format=api",
    "text_counter": 62,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Nilikuwa nimewaahidi wakenya kwamba leo tutazungumza kwa Kiswahili, maanake nilitarajia kwamba Mswada wangu wa kuzungumzia maswala ya vile ambavyo wakenya walidhalilishwa kule Tanzania utakuwepo leo. Hata hivyo, wacha nizungumzie Taarifa hii ambayo imeletwa na Sen. (Dr.) Boni Khalwale. Nawasikia wenzangu wakizungumza na kujipiga kifua kwamba SHA inafanya kazi. Kwa mtazamo wangu, kama hiyo SHA inafanya ni wananchi watatuambia, sio nyinyi viongozi kwa sababu hapa hamna mtu yeyote ambaye anapokea matibabu akitumia SHA. Kwa hivyo, ukisimama hapa na useme kwamba SHA inafanya kazi, tuoneyeshe ni lini ulitibiwa na SHA. Jambo la pili, wakati tulipokuwa tunazungmzia huu Mswada, tulisema kwamba tungependa kuwapa nafasi wale ambao walikuwa wanafanya kazi katika Shirika la NHIF ili wasifurushwe kazini. Mimi mwenyewe kama Seneta wa gatuzi la Nairobi, nilileta mabadiliko katika Mswada ule unaosema kwamba wale ambao wako pale, wapewe nafasi za kwanza kufanya mahojiano tena. Lakini, hawa hawa viongozi ambao sasa wanajipiga kifua wakisema tuwalinde wale wafanyakazi, walipiga kura kuhakikisha kwamba mabadiliko hayo hayakufaulu. Ni unafiki mkubwa ninapo wasikia watu ambao walikuwa na fursa ya kuhakikisha kwamba wafanyakazi hawa watapata haki wakipiga kura njia nyingine, kisha leo wanapata sauti na kutuambia kwamba SHA inafanya kazi. Bw. Spika, nina watu pale ndani ya Shirika la SHA wanaoniambia kwamba hata hizi interviews wanazofanya za kuwapa watu kazi, ni za bandia, maanake tayari wale ambao wanaenda kupewa hizi nafasi wanajulikana---"
}