GET /api/v0.1/hansard/entries/1566858/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1566858,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1566858/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Jambo la kwanza ni kwamba ipo haja kuwa na sheria ambayo itasaidia kaunti zetu kupata fedha ambazo zinapelekwa kwa Serikali ya Kitaifa na baadaye zinarudi kwa kaunti. Kwa mfano, faini zinazotozwa katika mahakama zetu kwa makosa kuhusiana na sheria ambazo zinasimamiwa na kaunti. Kuna sheria kuhusu ujenzi, wale wanaouza bidhaa kwa rejareja bila vibali na sheria nyingine kama hizo. Pesa hizo zinalipwa kwa Serikali ya Kitaifa inayokaa nazo kwa zaidi ya mwaka kisha baadaye inaleta Mswada Bungeni ili upitishwe. Kwa mfano, pesa zitakazopelekwa mwaka huu zilikusanywa mwaka 2022. Ipo haja ya kuhakikisha kuwa pesa hizo zinaenda moja kwa moja katika akaunti za kaunti zetu ili ziweze kutumika katika mwaka ambao zimekusanywa."
}