GET /api/v0.1/hansard/entries/1567450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567450,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567450/?format=api",
"text_counter": 477,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bwana Naibu Spika kwa kunipa ruhusa nichangie mjadala unaoendelea kulingana na uchunguzi uliofanywa na Kamati ya Afya kuhusu mtoto aliyefariki katika MTRH. Tumesikia mambo mengi hapa Kenya katika mfumo wa hii serikali ya Kenya Kwanza. Tumekuwa tukipigania wizara zote na hasa Wizara ya Afya iwe ikipata pesa nyingi kuliko wizara zingine zote. Huu ni wakati katika ulimwengu ambapo masuala ya afya yanaangaliwa. Serikali ya Kenya Kwanza imekuwa ikirekebisha mambo mengi iwe kwamba Social Health Authority (SHA) itakuwa ikifanya kazi usiku na mchana ili kila mtu akae maisha yanayofaa. Katika nchi za ng’ambo, mambo ya afya huangaliwa kupita mengine yote tangu kuzaliwa mpaka uzeeni na hata kufariki. Sote, hata mimi nikianguka hapa saa hii ni"
}