GET /api/v0.1/hansard/entries/1567452/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567452,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567452/?format=api",
"text_counter": 479,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "lazima nisaidiwe na daktari.Tunajiuliza, kama mambo haya yanatendeka katika hospitali kubwa, je, mashinani kwa mwananchi, ni wangapi wameteseka na kuumia? Tunajua wakati huu kuna shida za fedha na hospitali zinahitaji fedha. Jana tulilkuwa tunajaribu kupitisha hela za malipo ya madaktari yaliyochelewa. Ni mpaka tuwe na utu kwa madaktari kwa sababu tunapoomba tunaamini daktari ni kama Mungu wa pili. Hata kama kuna dawa, huwa tunaomba Mungu asaidie na pia aongoze daktari ili ajue mtu ameugua wapi au atapewa dawa zipi. Naomba tuangalie ili uchunguzi ulete mwelekeo na ukweli. Pia, familia hii ihudumiwe kwa njia ifaayo. Huenda ikawa familia itapata fidia ya pesa lakini uhai ulioondoka hautarudi ulimwenguni. Yafaa tujiangalie tukiwa human beings, awe ni daktari ama mtu yeyote. Daktari ni mtu muhimu sana. Kwa muda wa miezi miwili sasa, madaktari wamekuwa wakija katika lango la Seneti na tumekuwa tukiongea nao. Hata kama kuna shida ya hela, tunaomba madaktari muwe mkiangalia binadamu kwa sababu pesa haziwezi kulinganishwa na kazi mnayofanya. Ni mpaka muwe na roho ya Mungu na muwe mkisaidia binadamu. Bw. Naibu Spika, kuna magonjwa mengi katika ulimwengu. Binadamu ana shida nyingi na stress. Hata kama familia hii itapata fidia ya pesa haiwezi kuridhika. Madaktari hata kama wako na shida waangaliwe ili hospitali zetu za kaunti zipate dawa na pia ziwe na vifaa vya kazi na vile vitu vingine vinahitajika. Bw. Naibu wa Spika, kule mashinani, kuna shida nyingi. Magavana wako na shida na wizara pia ziko na shida. Miezi miwili iliyopita, Serikali ya Kenya Kwanza iliweka Waziri wa Afya na tunaona vile anajaribu kulainisha maneno ya afya. Karibu wiki mbili zimezipita, ninakumbuka kuna Director General aliyeajiriwa kwa hiyo Wizara. Kwa hivyo, ni mambo mengi yanayofa kuangaliwa. Hata kama pesa si nyingi, ningeomba daktari yeyote ule, awe mkubwa au mdogo, aliye kazi usiku au mchana, waangalie mambo ya binadamu. Kulikuwa na kisanga kule kaunti ya Embu Hospitali ya Level 3 miezi miwili iliyopita. Pia, miezi minne iliyopita, kulikuwa na kisanga kingine katika hospitali ya Kiritiri Level 3 ingawaje, huyo mtoto hakufariki. Huo wakati, mama alikuwa karibu kupata mtoto na hakuna daktari alikuwa karibu. Hakuna askari alikuwa karibu na hakukuwa na stima pia. Mambo ya ajabu ni kuwa yule mama alijifungua lakini watu wengi na familia nyingi zimeteseka. Huenda ikawa hawa watakuwa na fikira ya kushtaki kitendo kama hiki lakini vitendo vingi vimefanyika. Bw. Naibu wa Spika, jana nikiangalia kwa mitandao, kuna kisanga kingine kilifanyika. Kuna mama alikuwa anapata mtoto na kwa bahati nzuri, kulikuwa kina mama wanampeleka hospitali. Alilemewa kwa njia na kulikuwa na kijana, mwenyewe hiyo familia. Alipoonyeshwa kwa runinga, alisema alikuwa anapeleka bibi yake hospitali kupata mtoto na kufanyiwa upasuaji. Huyo kijana alikimbia, mambo ya ajabu lakini sikuangalia ile video vizuri. Alisema alikimbilia kule hospitali na daktari akamwambia ana kazi nyingi. Lakini baadaye, yule kijana akapewa vifaa vyote vya kuzalisha. Wale kina mama walikuwa karibu, walitoroka na yule kijana alisaidia yule mama kupata mtoto. Bw. Naibu wa Spika, akina mama wengi wajawazito wameteseka. Kwa hicho kitendo cha jana, watu wengi hawajahudhuria vile madaktari wanafanya kazi. Wanaume"
}