GET /api/v0.1/hansard/entries/1567454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1567454,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567454/?format=api",
    "text_counter": 481,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wengine, hata sisi wazee, tuko na uoga. Inamaanisha ya kwamba, kitendo kama hicho kiko kwa mitandao, katika ulimwengu huu na binadamu ameletwa na Mungu, mambo ya afya yanafaa kuangaliwa na ile njia inafaa. Mambo ya ajabu, huku Kenya na pia ulimwenguni, ni watoto wangapi wanafaa kuwa Seneti, kama wewe au mimi ambao wameondoka humu ulimwenguni kwa njia ambayo haifai kwa sababu, mtoto amezaliwa kwa njia? Huku Kenya yetu, tuko na shida. Tukiachana na mambo ya madaktari, utakuta mahali pako mbali na hospitali, barabara ni mbaya. Mvua ikinyesha na kuna mama mjamzito, akipata mtoto usiku, hakuna gari au boda boda ya kumsaidia. Mambo mengine hata kama tunaangalia, tungeomba Serikali ya Kenya Kwanza ipatie wizara zote pesa ili barabara zitengenezwe. Pesa ikipatikana na barabara zitengenezwe, magavana pia wapeleke wizara ya afya kule mashinani ili kusaidia wananchi. Bw. Naibu wa Spika, ninashukuru Serikali juu ya Community Health Promoters"
}