GET /api/v0.1/hansard/entries/1567456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1567456,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567456/?format=api",
    "text_counter": 483,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "sababu tunaona ile kazi wale wako mashinani wanafanya. Jana, tumepitisha fedha za CHPs na ningewaambia wasijali, pesa zao zinakuja na watalipwa fidia. Ningewaomba wafanye kazi kulingana na vile Mungu amewapatia. Tunajua kuna shida kwa sababu, asilimia hamsini inatoka kwa serikali za kaunti na hamsini hiyo nyingine inatoka kwa Serikali Kuu, lakini bado, pesa inakosekana. Ningeomba serikali za kaunti zipewe fedha za wale watu wako mashinani katika hospitali zote. Bw. Naibu wa Spika, tunajua kaunti nyingi hazina pesa za kusaidia mambo ya barabara, afya na mishahara, imesaidia ni kwa sababu sisi Maseneta, tunaongea mambo ya ugatuzi. Ndio maana tunasema, wakati mgao wa pesa utakuja, tungeomba kaunti zote zipewe pesa ambazo zinafaa. Na wiki ijayo, zile pesa zitapitishwa na Bunge, kaunti zilizo na shida, kama Embu na kule North Eastern, tutasema hakuna kaunti itapata pesa kidogo kuliko Shilingi 6 bilioni. Tutasikizana kutoka Shilingi 6 bilioni na hizo zingine, tuweze kuona vile tutaleta kaunti zetu pamoja. Tumeona kaunti nyingi zikifanya kazi na ziko na pesa nyingi, lakini hawangalii mambo ya audit . Mambo ya transparency yanatakikana kwa ugatuzi na pia serikalini. Tukifanya hivyo, watu wengi watafaidika. Watoto wengine wanazaliwa bila kufikisha miezi inahitajika. Utapata wengine wako miezi saba au nane. Ningetaka kusema, Bw. Naibu wa Spika, wazee waheshimu kina mama. Utapata mama ako na mimba lakini utapata kule nyumbani ni stress tu. Huyo mama ndiyo anaenda kutafutia watoto wale wengine chakula na kufanya kila kitu. Lakini huku Kenya, utapata mama wanakosana na mzee ilhali yule mama ni mjamzito na hii inafaa iangaliwe, ili tusaidie kina mama. Bw. Naibu wa Spika, nikimalizia, hata kama hii familia italipwa pesa, haitasaidia. Ningeomba pia, hata kukiwa namna gani, hiyo hospitali ama yule daktari aliyefanya hiki kitendo, tunajua wako na shida na pesa na mishahara lakini pia, walikubali kazi. Inafaa Serikali iwachukulie hatua ndio iwe funzo kwa madaktari wale wengine. Mimi kama “daktari” Alexander Munyi Mundigi, Seneta wa Embu, ninaunga mkono na haya mambo yaangaliwe na yalainishwe. Ningeomba SHA ifanye kazi katika hospitali zote na Wakenya wote wajiandikishe."
}