GET /api/v0.1/hansard/entries/1567643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567643/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzyo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": null,
"content": " Asante Bw. Spika. Kwanza, namuunga mkono ndugu yangu, Sen. Cherarkey, kwa Taarifa aliyoleta kuhusu vifo vya watu wa kanisa. Ni jambo la kusikitisha na huzuni na si sawa. Kanisa ni mahali ambapo tunaenda kumuomba Mungu. Vile vile, watu wakipatikana na shida ya aina yoyote, huwa wanakimbia makanisani ili kupata msaada wa maombi kutoka kwa mafather, mapastor ama wakuu wa makanisa. Bw. Spika, Father Bett alikuwa ameshikilia Bibilia kwa mkono alipopigwa risasi. Hakushikilia gongo, kisu au bunduki. Alishikilia Bibilia. Kwa hivyo, ni jambo la aibu na kusikitisha kuwa wale majangili waliingia pale ndani wakiwa na bunduki, wakampiga risasi na kumuua. Bw. Spika tunakemea vikali zaidi na tunataka kuona ya kwamba Serikali imechukua hatua hususan Inspekta Mkuu wa Polisi, Bw. Kanja, amechukua hatua mwafaka kuona ya kwamba waliofanya kitendo hicho wamefikishwa kortini. Vile vile, ningependa kusema kwamba si upande ya wakristu peke yake. Hata wale wakubwa wa kiislamu, masheikh kama vile Sheikh Aboud Rogo, alikuwa mkuu wa Msikiti Musa. Leo, hayuko nasi kwa sababu askari walisingizia. Hakuna ripoti au taarifa yoyote iliyoletwa kusema makosa ya Sheikh Aboud Rogo yalikuwa ni nini. Hakuna uchunguzi wa aina yoyote ulifanywa na idara ya uchunguzi kuonyesha Sheikh Aboud Rogo alikuwa na makosa gani. Leo hii, familia yake inalia. Wanataka kujua ni kwa sababu gani baba yao alipoteza maisha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}