GET /api/v0.1/hansard/entries/1567660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1567660,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567660/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "Hata kikao cha Seneti ambacho tunafanyia hapa wakati huu teknologia inatukubalia kuenda kule Kakamega, tuketi katika county assembly, tuzungumzie maneno ambayo ni yetu kama Seneti na pia tutembee mashinani na tuone vile pesa za wananchi wa Kakamega zinatumika. Tumetembea huko Garissa, tumeenda Wajir, na tumetembea mpaka Kisii na Marsabit. Tukifika pale tunaona ili magavana sasa wanaanza kujishughulisha, wengine wanaanza kutuzungumzia na wengine wanasema tutayafanya hayo mambo. Ningependa kusihi wale ambao mko hapa Seneti, mhakikishe kuwa kama tunatembea na tumeenda haswa kwa jimbo fulani, tuseme hivi juzi tulikuwa kule Machakos, tuhakikishe isizidi mwezi mmoja, tuwe tunaenda kuona yale ambayo tulikubaliana na gavana pamoja na maafisa wa kaunti yake kwamba yametendeka. Kama viongozi, ni lazima tuhakikishe hayo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}