GET /api/v0.1/hansard/entries/1567670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567670,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567670/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Sen. (Dr.) Khalwale kuhusu kucheleshwa kwa kumalizika kwa miradi kadhaa katika Kaunti ya Kakamega. Hili limekuwa donda sugu katika kaunti nyingi. Utapata Magavana wanaingia ofisini na kupuuza miradi iliyoanzishwa na magavana waliotangulia. Kwa mfano, kule kwetu Mombasa kuna miradi ya ECDE ambayo hivi majuzi tuliizuru tukiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu katika Seneti. Tulizuru ECDE ya Kengeleni ambayo ilianzishwa 2016, Chaani pia, 2016 na nyingine nyingi ambazo zimekwama. Hivi sasa wananchi wanalalamika kwamba hakuna huduma zinazotolewa katika majengo hayo. Wanakandarasi wanaendelea kupata shida kulipwa pesa zao kwa sababu miradi haijakamilika."
}