GET /api/v0.1/hansard/entries/1567679/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567679,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567679/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Taarifa iliyo wasilishwa na Sen. Eddy Oketch kuhusu visa vya ulaghai hasa katika benki ya Absa. Ninashangaa sana kwamba kama taifa tunapea benki leseni kufanya biashara na kulinda pesa ya wananchi wa Kenya, lakini wanarudi kuwalaghai na kuwaibia pesa. Itakuwaje mama kama huyo aliyestaafu pesa yake itoke katika benki Shilingi 2,498,029 na inasemekana waliohusika ni maafisa wa benki ya Absa? Ningeomba sisi kama Seneti inayolinda maslahi ya wananchi wa Kenya, tuite huyo mkurugenzi aje hapa atueleze kuhusu hivi visa tunavyoshuhudia, kwamba mtu akitoa pesa katika benki maafisa wanaofanya kazi pale ndio wanapigia wakora simu. Juzi nimeona katika meaneo ya magharibi mwa Kenya mtu ambaye alikuwa askari ameenda katika benki, ametoa pesa kwenda kulipa watu waliomfanyia kazi. Akitoka hivi tu, watu walio katika benki wanapigia wakora huko njiani. Hatuwezi kukubali wale ambao tumewapa jukumu la kutulindia pesa zetu wawe ndio walaghai wanaotunyang’ anya pesa yetu. Mimi ningetake nione sura ya huyo mkurungenzi mkuu wa Absa. Atasimamiaje pesa na awe katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba wafanyakazi aliowaajiri pale ni wakora? Tunataka kujua aliyesababisha mama Violet Akoth Nyator kunyang’anywa pesa. Je, yeye bado ni afisa kwenya ile benki ya Absa? Kama yuko pale si mwingine atanyang’anywa kesho? Kwani tutakuwa Seneti inayozungumza bila hatua yoyote kuchukuliwa? Tumwiteni mkuu wa kitengo cha kuchunguza uhalifu, DCI, aje hapa atueleza mambo haya tunayosoma kwenye magazeti. Nina ripoti nyingi sana nimesoma kwenya magazeti kuhusu watu waliotoa pesa kwenye benki na wakitoka, wale maafisa wa benki wanapigia wakora simu. Hii idara ya DCI imefanya nini kuwatia mbaroni wanaohusika? Mkuu wa Absa amefanya nini kuwaondoa wanaohusika katika visa hivyo? Hatuwezi kukubali kwamba wizi unafanywa kutoka ndani ya benki. Nchi itakuwa imeisha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}