GET /api/v0.1/hansard/entries/1567690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567690,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567690/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika kwa kunipa ruhusu nichangie na niwakaribishe watoto wa Kanyuambora Secondary School. Hii shule iko Mbeere North katika Kaunti ya Embu. Ni pahali ningetaka kusema ya kwamba, wakati wa by-election, tutakua huko. Kiongozi wa Wengi alikua amewakaribisha na ningeomba wakati wa siasa ukija, apitie kwa hiyo shule. Ni shule nzuri kule Embu na elimu inaendelea vizuri sana. Bw. Naibu wa Spika, hii shule imetoka Mbeere North, pahali hakuna maji, hospitali au vitu vingine. Ndio maana tumesema kwamba pesa za capitation zipeanwe shule ili watoto kama hawa wajikakamue, kwa sababu huko hakuna hospitali ama dawa na wakipata zile pesa zitawasaidia. Nikimalizia, hii shule iko pahali hakuna maendeleo. Hata walimu wakienda hiyo shule ni shida na ndio maana tukichangia tulisema hardship allowance isitolewe katika Kaunti ya Embu, Mbeere North na Mbeere South ili walimu washeherekee na watoto wetu waendelee vizuri. Bw. Naibu wa Spika, wakirudi nyumbani, ningewaomba wasijielemishe kuhusu mambo mabaya kama pombe na madawa ya kulevya, kwa sababu ni wao watakua maseneta, magavana au Spika, kama yule tuko naye siku ya leo."
}