GET /api/v0.1/hansard/entries/1567787/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567787,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567787/?format=api",
"text_counter": 269,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Korir",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia ripoti ya Kamati ya Afya. Napongeza Kamati kwa kazi nzuri walioifanya, wakiongozwa na Mhe. Mandago ambaye amekuwa Gavana wa Kaunti ya Uasin Gishu. Yeye anaelewa kwa undani kazi ya afya kwa sababu hii ni moja ya jukumu lililohamishwa kwa ugatuzi. Watu huenda hospitali kwa sababu ya afya yao na wana haki ya kupata matibabu yanayofaa. Wanafaa kuhudumiwa kwa njia inayofaa kwa kutumia teknologia inayofaa. Sio haki kwa mwananchi kupoteza maisha. Jepkorir ni mmoja wa wale walipoteza maisha yao kwa njia isiyoeleweka. Ni vizuri tuchunguze changamoto zinazokumba hospitali zetu za kaunti. Changamoto kubwa waliyonayo ni uhaba wa madaktari na ukosefu wa madawa na vifaa vinavyoweza kusaidia kuchunguza magonjwa mbalimbali. Ni kero kubwa kupoteza maisha kwa njia isiyoeleweka tunapoenda kutafuta matibabu. Mhe. Spika wa Muda, naomba Kamati ya Afya watembelee kaunti zetu kuchunguza huduma zinazotolewa kwa hospitali za kaunti. Juzi, nimeshtuka sana kuona mwanamume mmoja kule Murang’a akiwa amebeba maiti ya mtoto kifuani huku akilia kwa uchungu. Alikuwa amekaa na huyo mtoto siku nzima bila kupata usaidizi."
}