GET /api/v0.1/hansard/entries/1567792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1567792,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567792/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Korir",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "vifaa vya kusaidia madaktari kutoa huduma ama hawajalipwa mishahara yao ambayo inawapa motisha ya kuendelea kutoa huduma zao. Lazima tutilie hayo maanani. Ingawa hata kama hujalipwa vizuri, hakuna mtu anayefaa kupoteza maisha. Nakubaliana na pendekezo kuwa familia ya mwendazake ilipwe fidhia. Hata hivyo, pesa zitakayolipwa haziwezi kulinganishwa na uhai wa binadamu. Vile vile, Kamati hiyo inapendekeza kuwa ripoti ya jinsi watakavyokubaliana na familia hiyo iletwe hapa. Hiyo pia haitoshi kwa sababu walishapoteza mtu wao. Tunafaa kuwa na njia kuhakikisha kwamba kuna utaratibu katika kaunti zetu. Bi. Spika wa Muda, sitaki kusema mengi. Mwisho ni kuwa tunafaa kuendelea kuangalia kwa undani mambo ambayo yanakumba serikali za kaunti ili tuweze kuyashughulikia na kusaidia watu wetu wasipoteze maisha yao."
}