GET /api/v0.1/hansard/entries/1568042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1568042,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1568042/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohamed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Namuunga mkono ndugu yangu Mhe. Junet Mohamed kwa kusema kuwa Kenya ni yetu sisi sote. Inasikitisha kuwa Bw. Gachagua hajakubali kuwa hako kwenye mamlaka tena. Ikiwa kitu kikitolewa kwa Wakenya wote ni udhalimu lakini kikitolewa kwa sehemu moja ni furaha yake, basi anakosea Wakenya. Nikimnukuu, alisema: “Hii Kenya, ikiwa mtu mwingine ataingia katika uongozi, taharuki ya mwaka wa 2007/2008 itakuwa kama harusi. Kitakachofanyika kitakuwa balaa zaidi.” Jamani, huyu ni mtu kweli? Nataka nimwambie Gachagua kwamba nchi hii si yake peke yake. Usipotoshe Wakenya. Ulikuwa ukituambia wewe ndiye mlinzi kwenye mlango. Ulikuwa ukituambia vitu vilivyofanyika vilikuwa sawa. Leo hii, kwa utepetevu wako, uko nje ya Serikali kwa kunyang’anya wajane na mayatima haki zao na kufanya siasa za hisa. Wakenya wakasema: “Toka nje.” Leo unaanza siasa za kugonganisha Wakenya. Ninaona ameshikana na Mhe. Ndindi Nyoro. Kuna siku nililalamika hapa kwa sababu ya shida ya mafuriko kule Mombasa. Nikalia sana hapa lakini hatukupata pesa za kuhimili majanga, ama disaster preparedness kwa lugha ya kimombo. Na Mhe. Ndindi Nyoro akanionyesha shilingi billion 4 za World Bank ambazo ziliwekwa kwenye bajeti ya Ofisi ya Naibu Rais wa wakati ule, Gachagua, na akaniambia ameziramba. Akanionyesha shilingi bilioni 6 ambazo zilikuwa katika bajeti na akaniambia Gachagua ameziramba . Leo yeye ndiye anarudi huku nyuma, kwa sababu tunaambiwa kwamba nyani akikosa ndizi husema mgomba umeteleza. Haiwezekani. Kama wao ni wendawazimu, waache wale ambao wako na akili zao waweze kuongoza Kenya. Leo tuko na Naibu wa Rais anayefanya kazi. Anazunguka huku na kule na tunaona anafanya maendeleo na Wakenya wanafurahia. Sisi hapa tulikuwa tunampinga Rais na leo tumeaibika kwa sababu gani? Ule ushuru wa nyumba tulikuwa tunalia kuhusu, leo tumeona The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}