GET /api/v0.1/hansard/entries/1568044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1568044,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1568044/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohamed",
"speaker": null,
"content": "watu wameingia kwenye nyumba za kisasa. Wametoka kwenye vibanda . Ilikuwa ni uchungu kwa sababu hii Kenya uchumi umekuwa mbaya na kila mtu alikuwa anasikia uchungu wa uchumi. Lakini mimi leo nampongeza Rais. Ndiyo, alitufinya, lakini sasa tunaona kupitia Social Health Authority (SHA), yule maskini, tajiri na wote wanatibiwa. Upande wa makazi, maskini na matajiri wanakaa vizuri. Unga sasa imeshuka bei, na mafuta yameshuka bei. Mheshimiwa Spika, Rais anaipeleka Kenya vizuri kwa sababu amepata kile kikosi ambacho kimemuongezea nguvu na sasa anafanya kazi vizuri. Namwambia Rais asimwangalie yule mwendawazimu aliyemfurusha kule Ikulu. Rais aangalie kazi yake. Yule mwendawazimu tutamshuhulikia. Mimi namngoja Mombasa kule na ananijua. Hawezi kuja kutuchafua kule Mombasa. Hatuwezi kukubali. Tunataka Kenya ambayo ina amani. Tunataka Kenya ambayo itasonga mbele bila bugdha. Mhe. Gachagua aangalie, ajiite mkutano ajiulize. Amekuwa kama yule mtoto ambaye wageni wakija myumbani unamficha kwa sababu ataharibu. Mpe kipaza sauti tu kidogo, ashaharibu kila kitu. Kama juzi, alienda kuchapa wale wasanii ambao walikuwa wanamsaidia . Leo amewachapa. Kesho atafanya mengine na mengine. Kwa hivyo, sisi tunasema Rais ashike kasi. Sisi tuko ndani ya Broad-Based Government na tutakusukuma mbele. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}