GET /api/v0.1/hansard/entries/1568433/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1568433,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1568433/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kuniruhusu kuchangia kwenye Ripoti hii ya Kamati kuhusu ripoti ya Auditor-General kuhusiana na State corporations. Ukiingalia Ripoti hii, ni dhahiri shahiri kuwa pesa nyingi za taifa zinapotea kwa sababu ya kuzembea kwa wale wanaohusika katika hizi State corporations tofauti. Ukiangalia hata mashamba, mfano kwenye KBC, KEMSA na mashirika mengine mengi, mashamba ambayo wanafaa kutumia kwa ujenzi na kuendeleza miradi tofauti ya Serikali hayana vyeti vya umiliki. Nikitoa ushahidi dhahiri ni kuwa hata Mombasa, kuna wakati tuliizuru Idara ya Maji na tukapata kuwa wanashamba wanadai kuwa shule ya msingi ya Nyali imechukua shamba lao lakini wakiulizwa cheti cha umiliki, hawana ilhali wenye shule wanacho. Hivyo, unajiuliza, je, Serikali ilienda kwa watu bila vyeti vya umiliki, au watu walizipataje ilhali Serikali haina? KEMSA pia wako katika hilo kundi. Wanamashamba wanadai ni yao ila hawana vyeti vya umiliki. Kenyatta National Hospital (KNH) pia ina mashamba ambayo wanasema ni ya Serikali bali hayana vyeti vya umiliki. Ninaomba kuwa, ikiwa tunaweza kuchukua hivi vyeti vya umiliki vyote na kusihi Wizara ya Fedha kushugulikia ili wapate vyeti vya umiliki vya Serikali katika wizara moja, itasaidia sana Serikali. Hii inasababisha sisi kama ukanda wa Pwani, kuwa na matatizo ya mashamba sana. Kuna watu wameishi huko kwa miaka zaidi ya mia, lakini wanavunjiwa nyumba zao na kuambiwa shamba ni la wizara wakati ambapo wao wenyewe wamekaa pale kwa miaka yote. Ndio maana nampongeza Rais kwa kutuwekea Ksh1.5 billion ya kufidia mashamba ya wale wasiokuwa na vyeti vya umiliki ilhali wamekaa pale kwa miaka mingi, ili wapate vile vyeti. Hii itatoa sintofahamu iliyokuwepo baina ya wananchi na Serikali ama hata na wale wezi wa mashamba. Mtu anaenda pale Ardhi House, anaangalia sehemu fulani haina cheti cha umiliki, anahonga humo ndani na kuchukua hiyo hati miliki na kuenda kugawia watu. Mhe. Naibu Spika, nikiangalia Ripoti hii, pesa nyingi sana zinafujwa na hata mhasibu anakuwa mzito kutoa zile rekodi kwa sababu anajua kuna kitu fulani kimefanyika. Wakenya watamlaumu Rais na viongozi wa juu kila wakati kumbe humu ndani na chini kuna watu ambao wanafanya makatafunwa yao. Kwa mfano, bado National Hospital Insurance Fund (NHIF) inadaiwa na KNH. Unashangaa iwapo hili shirika lilisongezwa na kuingizwa kwenye Social Health Authority (SHA). Juzi, Rais ametueleza wazi kuwa kwenye miaka 50 ya nyuma, idara kama NSSF imekusanya karibu Ksh300 billion pekee. Alipokuja mamlakani aliweka mikakati mizuri ikawa wakenya wanalipa Ksh600 katika National Social Security Fund (NSSF). Kwa sasa, Kenya imekusanya kiwango mara dufu. Pia alituambia kuwa hizi hazina ambazo tunajiwekea sisi wenyewe zitakuja kutusaidia badala ya kukopa Uchina na nchi zingine pesa na kuanza kuweka vitu vyetu kama bandari. Tutakuwa tunajikopa na kujilipa sisi wenyewe. Hivyo nampongeza Rais kwa juhudi zake. Lakini nawaomba wanaohusika huku chini waache wizi ili wasiharibie taifa hili jina. Mwisho, kwa niaba ya wakenya, namuomba Mhe. Rais Salmia Suluhu msamaha. Watoto wetu wamekosea. Nyinyi ni mjirani wetu hivyo tunaomba msamaha. Tukae tukipendana kwa wema kama taifa. Ahsante, Mhe. Naibu Spika."
}