GET /api/v0.1/hansard/entries/1568934/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1568934,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1568934/?format=api",
    "text_counter": 392,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Niseme kwa huzuni kwamba sisi viongozi Wajumbe tuna jukumu la kuhakikisha kwamba sheria ambayo tunaipitisha, inaidhinishwa, kupitishwa na kutumika vizuri. Pia, wakati tumeteuliwa kama wenyeviti wa kamati, na tunajua kuwa imekuwa vigumu kwa mawaziri kuletwa hapa… Hata wakiletwa hapa huwa kwa masuala mengine na inabidi wakati tunaenda kuwauliza, nasi pia tufanye upelelezi wetu ndio tukija kujibu, tunajibu maneno ambayo tunajua yanastahili kujibiwa kwenye Bunge hili. Ninasema hivyo kwa sababu watu walikufa. Watu waliuawa. Sio kule kuuawa eti pengine unampiga mtu risasi kwa mguu halafu anavuja damu mpaka afe, ama amepigwa tumboni ndio labda baadaye aende afe hospitalini. Watu watano waliuawa na wanne walipigwa risasi kichwani. Hii ni kumaanisha kwamba kulikuwa na amri ya kupiga risasi ya kuua sio ya kuumiza; piga risasi, ua. Sio mimi niliuliza hilo swali, but ordinarily, swali likiulizwa kwenye Bunge hili, linakuwa property yake. Kila Mjumbe anastahili kuliongelelea na kuuliza kama hilo swala limejibiwa vizuri. Ninaamini kuwa Mhe. Julius Sunkuli, ambaye ni jirani yetu mwema, alitaka kujua lakini sio sana mambo ya ardhi kwa sababu yameulizwa Kamati husika. Swala hili liliulizwa Kamati inayohusika na usalama wa nchi ya Kenya. Yale maneno yote tumeambiwa hapa ni kuhusu wale watu watano ambao waliuawa. Je, Idara ya usalama imechunguza mpaka iko na post mortem ya kuonyesha kuwa hawa watano waliuawa kivipi, na bunduki gani, na risasi ya nani iliua hawa watu? Saa hii tungesomewa list ya wale askari ambao waliua hawa watu. Hapo ndio nafikiri hata Mheshimiwa mwenyewe alitarajia hilo swala lijibiwe: ni akina nani waliua hawa watu na ni hatua gani Serikali imechukua dhidi ya wale ambao waliua hawa watu? Tumeona mambo mengi yakiendelea Kenya hii. Kuna mambo ya kushika watu, wanasiasa na watu ambao wanafanya mambo kidogo kidogo sana. Lakini ikifika mahali ambapo polisi wenyewe wamefanya makosa, kama haya yalifanywa Angata Barrikoi, hata saa hii tukiongea, wacha hata kukamatwa, kusimamishwa kazi ama kupigwa transfer … Hawajapigwa transfer mpaka wa leo tukiongea - askari, DCC na mwenye alipeana orders . Tunashangaa na hili ni swala ambalo Chairman anafaa kuliangalia vizuri. Nani anapeana"
}