GET /api/v0.1/hansard/entries/1569853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1569853,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569853/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Swali langu la kwanza lilikuwa – kwa takwimu, Waziri apeane zile ada na kodi zote ambazo zinalipwa na wakulima wa majani chai. Nimeona kwamba amejibu na kusema vile Serikali inafanya. Haya yote wanayofanya ni sawa, lakini hakulijibu swali langu. Kulingana na nakala nilizonazo, mkulima wa majani chai, kutoka Serikali kuu mpaka zile za ugatuzi, analipa ada na kodi tofauti tofauti 42. Na nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi tulikuwa tumekaa chini na tukaelewana kwamba Serikali itajaribu kuzipunguza. Lakini kwa sababu ambazo sijaelewa, Bw. Waziri hakuziweka wazi. Kwa hivyo, Bw. Spika, kwa swali hilo, sikuridhika na majibu ambayo Bw. Waziri amepeana. Hii ni kwa sababu nilikuwa ninatarajia kama ni taasisi ama halmashauri ya kuchukua kodi, inachukua kodi zaidi ya tano. Halmashauri ya NEMA na taasisi ya AFA zinachukua kodi. Ili tuweze kulijibu swali hili na kuendelea mbele, ninamwomba Bw. Waziri alijibu hili swali. Swali langu la pili ni kwamba, katika Bunge la Kitaifa, kuna nakala ambazo Bw. Waziri alizipeleka pale mwaka huo ambazo zilikuwa zina kodi mpya ambazo zilikuwa zinafaa pia kutozwa wakulima wa kahawa. Hiyo sheria bado iko katika Bunge la Kitaifa. Niko na nakala hapa ambayo ilichapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Ningependa kumwuliza Bw. Waziri – kilimo cha msingi, kitatozwa ushuru mpaka lini? Katika nchi ambazo zinaendelea, kilimo cha msingi hakitozwi ushuru ili mkulima aweze kunufaika na kilimo chake."
}