GET /api/v0.1/hansard/entries/1569967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1569967,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569967/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza, ninakupongeza kwa kazi unayofanya. Tunashukuru. Kuna hatua ulichukua sehemu ya Tana River na ukasimamisha uchimbaji wa madini ya gypsum. Tulitarajia kwamba utafuatiliza, uweke mikakati ili wale wananchi wanaofaidika kwa uchumi huo wa uchimbaji wa gypsum, wawekezaji na serikali ya kaunti wapate haki yao. Baada ya hatua ile ambayo sote tuliipongeza, Serikali ya Kitaifa kutoka kwa ofisi yako mmenyamaza. Sisi na watu wa Tana River tungependa kujua kunaendeleaje na mipangilio ni namna gani? Pale pia palikuwa kitega-uchumi na watu, hali ndizo hizi, wanataka kuishi."
}