GET /api/v0.1/hansard/entries/1569984/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1569984,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569984/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, nami niulize swali langu. (a) Je, Wizara imeweka mikakati ipi kuhakikisha ya kwamba wavuvi nchini Kenya wamepata mafunzo ya kisasa ile kuongeza mapato yao? (b) Je, Waziri anaweza kutoa maelezo kuhusiana na utumizi wa Shilingi 1 bilioni zilizotolewa na idara ya masuala ya kimataifa ya Serikali ya Canada, Global Affairs Canada, kufadhili mradi wa wananawake wanaoshiriki katika biashara za baharini, maarufu kama Investing in the Women in the Blue Economy in Kenya (IWBEK) project in Kenya na kuweka wazi majina ya kampuni na vikundi vilivyofaidika, kaunti wanazotoka, waliofaidi, fedha walizopokea na ni lini walipokea fedha hizo? (c) Je, Waziri anaweza kueleza ni hatua gani zinazochukuliwa na chuo cha bandari, Maritime Academy na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, kuhakikisha kuwa vyeti vya mafunzo vinavyokabidhiwa na chuo hicho, vinapata utambulizi kamili wa kimataifa. Asante."
}