GET /api/v0.1/hansard/entries/1569987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1569987,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569987/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Hon. Hassan Ali Joho): Asante, Bw. Spika. Wizara kupitia idara ya jimbo la Uchumi wa Blu na Uvuvi imeshiriki kikamilifu kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wa Samaki katika uvuvi wa Bahari kuu kwa ajili ya kuzalisha ajira. Vile vile, Wizara imetoa uwezo wa kuwapatia bidhaa za uvuvi kama maboti na ujenzi wa bandari ndogo za uvuvi na bidhaa nyinginezo zinazostahili kuboresha biashara ya uvuvi katika maeneo ya jimbo la Pwani na katika maeneo ya Lake Victoria na Turkana. Swali la pili ni kuhusu pesa za ku-empower akina mama kupitia shirika la NGO kutoka nchi ya Canada. Ripoti ambayo niko nayo ni kwamba shirika hili lilitumwa likatafuta pesa kutoka Serikali ya Canada ama wafadhili takriban Shilingi 1 bilioni. Baada ya kutafuta hizo pesa, walianza kupeana grants ama msaada kwa vikundi vya akina mama vilivyomo katika jimbo la Lake Victoria na Pwani. Habari ambayo Wizara iko nayo ni kwamba walifanya vetting wakatambua beneficiaries na wakapeana mpaka sasa takriban Kshs403 milioni kwa vikundi tofauti tofauti, vikiwemo vikundi vya Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamu, Busia, Siaya, Kisumu, Homa Bay na Migori. Ningependa kuwaambia kwamba NGO inavyofanya kazi, hawahusishi sana vyombo vya Serikali. So, hatujaweza kupata the detailed expenditure ama vile zile pesa zimetumika kikamilifu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}