GET /api/v0.1/hansard/entries/1569996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1569996,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569996/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Swali langu ni, jamii za Pwani ambazo zinategemea uchumi samawati ikiwemo uvuvi na fedha ambazo zinashirikiana na bahari, tunaona kwamba hundi zinapeanwa mara nyingi na hata Rais anapokuja Pwani, tunaona miradi nyingi anazosimamia ni miradi ya uchumi samawati. Lakini kila wakati tunapouliza fedha zile zinawafikia kina nani, hatupati majibu. Leo, Waziri amesema wazi ya kwamba hawana ufahamu ni akina nani wamekuwa wakipokea pesa hizi. Je, tutawaambia nini Wapwani kuhusiana na zile hundi za fedha ambazo tunaona zinaendelea kupeanwa na hatujui wanaozipokea ni akina nani? Pili, kwenye upande wa uvuvi, ningependa kumwuliza Waziri, ndugu zetu wanapopata ajali katika maji, wanapozama wakiwa kazini wanavua, kuna mikakati gani kuona kwamba wanapata chombo kama helicopter, ili wakati ajali zile zinatokea, wanaweza kukimbia na kuwapa huduma ya kwanza haraka? Asante, Bw. Spika."
}