GET /api/v0.1/hansard/entries/1570000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1570000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570000/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Miradi iko tofauti ya uwazi wa Serikali na vyombo visivyokuwa vya Serikali. Hii Shilingi 1 billioni ambayo umesema ni pesa ambayo imepitia NGO, wamepata rasilmali kupitia Serikali na ufadhili wa Canada. Imekuwa changamoto kwetu kuwauliza hii NGO itupatie hesabu na uwazi kwa sababu wako na tabia na mienendo zao. Lakini zile za Serikali, niko tayari kueleza kinaga ubaga kwamba tumepeana takriban Shilingi 3.2 billioni kwa vikundi tofauti vya akina mama na vijana, kunua maboti. Tumenunua maboti takriban 129, tumejenga bahari za uvuvi chache, tisa hivi. Wakati huu tunajenga katika Lake Victoria, tumejenga zingine tano katika jimbo la Pwani, zingine bado zinaendelea, zingine tumeadvertise juzi na kadhalika. Kuhusu jambo la ajali, ningependa kusema kwamba wale watu ambao unawaita watu wako ni watu wetu sisi wote. Kwa sasa hivi, ukienda Lamu, Mombasa, Kilifi na Kwale, utakuta tumewapatia boti la kuokoa watu la uwepesi, lenye mwendo wa kasi, la kisasa. Lakini, ninakubaliana na wewe kwamba katika mipango za siku za usoni, tunataka kuekeza katika teknolojia mpya ya kutumia drones na helicopter. Hiyo iko katika mipango kabambe ambayo tumeweka. Tukitathmini kwa kina, utakuta kwamba hiyo ndiyo njia mwafaka ya kufuata."
}