GET /api/v0.1/hansard/entries/1570011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570011/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, kulingana na nakala ambayo tumepewa na Waziri, kuangalia zile kaunti ambazo zilifaidika na ule mgao ambao ulikuwa umepewa, hata kama ilikuwa ni fedha ya mashati kutoka Canada, kuna baadhi ya maziwa makubwa na mojawapo ni lile Ziwa la Turkana ambao pia wako na matatizo yao na wangependa kufaidika. Kwa kuwa hawakuwa katika orodha ambayo tuko nayo siku ya leo, ni mipango gani uliyo nayo kuhakikisha kwamba wale wenyeji wa Kaunti ya Turkana na Marsabit ambao ndio wenyeji wa Ziwa Turkana wanafaidika pamoja na maziwa mengine 23 ambayo tunayo hapa Kenya? Asante."
}