GET /api/v0.1/hansard/entries/1570351/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570351,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570351/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ambayo tulikuwa tumepitisha katika Jumba la Seneti ya kupatia gatuzi zetu takriban shilingi bilioni 465, imeangushwa katika Bunge la Kitaifa. Mara nyingi, huwa nasema machozi ya mtengeneza jeneza hayaaminiwi kwenye matanga. Wakati mwingine huwa wanakuja biashara ila si kuhuzunika na waliofiwa. Wale waliomo katika Bunge la Kitaifa pia wanafaa wajue kwamba wakati mtu anawania kiti chochote, anawania akijua ile fedha atakayopata atafanya nayo nini. Kwa hivo, tunapojaribu kupata pesa zaidi kuenda katika gatuzi zetu, lakini inapofika katika Bunge la Kitaifa DORA iliyopitishwa inaangushwa, inaonyesha ya kwamba adui wa ugatuzi ni akina nani. Kwa hivyo, tunarudi pale pale tulipoanzia. Bw. Spika wa Muda, nimetoka Kaunti ya Kirinyaga. Mimi ni Seneta wa Kenya kutoka Gatuzi la Kirinyaga. Hata hivyo, itakuwa sijafanya haki kama sitaongea kuhusu Kirinyaga pia nikiongea kuhusu gatuzi zingine katika nchi ya Kenya. Tunapopata fedha ambazo tunapata miaka ambayo imesonga, tukitoa ile fedha ambayo inafaa kulipa mishahara na mambo kama hayo, pesa inayobakia kufanya maendeleo huwa ni finyu sana. Mwamba ngoma wakati mwingine ngozi huvuta kwake. Ukienda katika eneo ambalo lina ukubwa, robo tatu katika Kirinyaga County, iko sehemu ambayo inakuzwa mpunga. Ni kubwa mno lakini mashamba na njia za kupitia kwenda kwa yale mashamba toka tupate uhuru haijawahi guzwa, kwa sababu pesa tunazopata ni kidogo mno. Nikiruhusiwa, hizi gatuzi ndogo tujiite wadogo kama sisi kwa sababu sisi ni kama wadogo wenu. Ndio maana nawasihi wakati meza ya chakula cha jioni ama meza imewekwa, imetengenezwa ili watu waweze kukula kwa ile meza na uko na ndugu mdogo amabao hawafikii meza. Si vibaya kumpatia tonge angalau pia akue ili siku moja aweze kukaa na wewe katika meza mkule pamoja. Bw. Spika wa Muda, kwa mfano, tuagazie kaunti ya Elgeyo Marakwet ambao Bajeti ya mwaka waliyopewa juzi waliweza tu kununua tinga tinga moja la kulima"
}