GET /api/v0.1/hansard/entries/1570355/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570355,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570355/?format=api",
    "text_counter": 246,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nikisema hivyo, itakuwa ni madharau kwa sababu atakuwa amekanyaga juu ya meza. Tunataka tu kupewa anagalu tonge tuweze pia kukua na zile gatuzi ambazo zinafaidika zaidi. Vile vile, tunapotafuta hizi fedha, kuna mambo ambayo yanafanyika katika gatuzi zetu ambayo tunafaa tuyamalize pia. Tunapowapatia magavana pesa kwenda kwa ugatuzi, lazima wajue pia wako pale kwa sababu ya wale waliowachagua na kuna sheria za kufuata kwa sababu Katiba lazima ifuatiliwe. Mfungwa hachagui gereza. Kwa hivyo, lazima wafuate sheria. Mara nyinyi huwa tunang’ang’ana kupata fedha lakini zinapofikia magavana, wanaanza kuwa wajeuri na wakiitwa katika kamati hawaji, wakiulizwa maswali hawahjibu lakini sasa hivi, wanataka tuwapatie pesa. Najua kuna mpango na jamaa fiche hata zile pesa zinaokotwa katika Gatuzi la Kirinyaga katika malipo ya ndani kwa ndani kwamba nyingi zinapotea na kuibiwa. Kwa hivo, ni lazima magavana waajibike. Nikimalizia, ningetaka niseme ya kwamba fedha ambazo tunaomba katika zile kaunti ambazo si kubwa sana--- Wakati kigezo kimewekwa cha kuangalia wingi wa watu, hakuna kigezo kiliwekwa cha kusema msongamano wa watu katika kaunti ndogo. Hiyo ni kusema ya kwamba, unaweza pata kaunti ambayo iko na watu wengi kwa sababu ni kubwa lakini kuna kaunti zingine kama vile Kirinyaga ambazo ziko na msongamamo wa watu, yaani ni ndogo. Utapata kama kwa hekari moja wanaishi kama familia nne ama tano. Hii inakuja pia na shida zake za kupeana huduma kwa watu wanaoishi hapo. Kama vile Sen. Mungatana alikuwa amesema, kuna mambo ambayo tulikuwa tumeskizana kwamba, katika mkutano uliokuwa asubuhi, tuangaliliwe hata kama ni kidogo tuweze kukaribia wale wakubwa wetu ambao wako na gatuzi kubwa. Kwa sababu mbuzi wa kuazimwa au kupewa haangaliwi meno. Kile ambacho tutapata, tutaridhika zaidi ili iweze kunufaisha wananchi wetu ambao wako mashinani. Bw. Spika wa Muda, nashukuru Mwenye Kiti wa Kamati ya Seneti ya Fedha na Bajeti kwa kazi nzuri waliofanya. Si kazi rahisi kuja na kuleta ile formula amabyo tumeiona hapa. Ingekuwa si vizuri kukaa na kukashifu ile kazi ambayo Kamati ya Fedha na Bajeti na Mwenye Kiti walifanya. Walakini, wakati mwingine kuna watu hata ukifanya nini hawaridhiki. Kuna mtu hata ukiogelea atasema bado unamtifulia vumbi. Kunao watu bila msingi wowote watakuambia wewe ndiwe sababu jangwa la Sahara halina nyasi. Kwa hivyo, kazi waliofanya kufikisha mahali tulipo, kuhakikisha kuwa hakuna gatuzi linapoteza pesa ni jambao ambayo anafaa apewe kongole. Asiulize kwa nini nisimwambie “hongera” kwa sababu “hongera” hupewa wanawake. Kwa hivyo, sisi tukipewa chochote hata kama ni chenye naona katika simulizi iliyoletwa hapa na"
}