GET /api/v0.1/hansard/entries/1570371/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1570371,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570371/?format=api",
"text_counter": 262,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ikumbukwe wazi kama vile Sen. (Prof.) Kamar alivyosema ya kwamba Seneti iliyopita kauli mbiu ilikuwa hakuna kaunti ingepoteza pesa. Huo ndio msimamo kwa sababu Katiba yetu inasema kazi ya Seneta ni kulinda na kutetea kaunti zetu. Sen. Mandago hatetei Uasin Gishu tu bali ana jukumu la kutetea kaunti zote za Jamhuri ya Kenya kwa sababu ni Seneta wa Kenya."
}