GET /api/v0.1/hansard/entries/1570372/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1570372,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570372/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nakumbuka Seneti iliyopita tuliketi hapa zaidi ya vikao kumi bila makubaliano, lakini dakika ya mwisho tulikubaliana. Mpangilio wa ugavi uliotumiwa katika muhula wa tatu wa ugavi, ndiyo huo unaotumika wakati huu. Wakati ule watu walijadiliana na mambo mengi yalifanywa. Kuliundwa Kamati iliyokuwa ikiongozwa na Sen. Sakaja na Spika wa Bunge la Kitaifa wakati huu, Mhe. Wetangula. Tuliongea mengi na kukubaliana."
}