GET /api/v0.1/hansard/entries/1570375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570375,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570375/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, kwanza kabisa ijulikane wazi kwamba pesa zinapaswa kufuata majukumu. Majukumu mengi yamepelekwa katika kaunti zetu lakini pesa zinabaki katika Serikali ya Kitaifa. Ikiwa hatutalivalia njuga jambo hili la pesa kufuata majukumu, tutakuwa tukipigania mkoba mdogo wa pesa, lakini mkubwa unao Serekali ya Kitaifa. Sisi tunapigana hapa lakini hatuwezi kufuatilia mahali palipo na hela kwa sababu majukumu mengi ambayo yamepelekwa katika kaunti zetu hayajafuatwa na pesa zake. Kwa Mfano, Mwenyekiki wa Kamati ya Afya yuko pamoja na sisi hapa. Hela nyingi za afya ziko katika Serekali ya Kitaifa ilhali Serikali imebaki na jukumu la sera na hospitali za kitaifa karibu tano ambazo ni Moi Teaching and Referral Hospital (MTRH), Kenya National Teaching and Referral Hospital, National Spinal Injury Referral Hospital, Kenyatta University Teaching and Referral Hospital na ile ya Mathari National Teaching and Referral Hospital. Hizo ndizo tu za Serikali ya Kitaifa ilhali asili mia 70 ya pesa zinabaki huko."
}