GET /api/v0.1/hansard/entries/1570376/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570376,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570376/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mfano kuhusu barabara, Katiba inasema barabara zimegawanya mara mbili, za gatuzi na za kitaifa. Hata hivyo kuna halmashauri na taasisi kama vile Kenya Rural Roads Authority (KeRRA), Kenya Urban Roads Authrotity (KURA) na Kenya National Highways Authority (KeNHA) ilhali hizo pesa zingepelekwa moja kwa moja katika gatuzi zetu kwa sababu kuna aina mbili pekee. KeNHA ingebaki ikishughulikia barabara za kitaifa ilhali KeRRA na KURA zipelekwe katika gatuzi zetu kwa sababu huwa wanashughulikia barabara zilizo katika gatuzi zetu."
}