GET /api/v0.1/hansard/entries/1570377/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570377,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570377/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tunapoongea kuhusu pesa ni vizuri tuwajibike vizuri na kusema kwamba gatuzi zinapaswa kuangaliwa. Kwa mfano hela zinazopewa kaunti ya Laikipia na majukumu tunayotakiwa kufanya pale, hizo hela ni chache sana. Hazitoshi. Kwa sababu leo asubuhi tulikuwa na huu mdahalo wa kujadili tutakavyoweza kuongeza hela zinakwenda katika kaunti ndogo kuliwekwa Kshs2 billioni kama hatua ya kuleta pesa za usawazishaji. Hizo fedha ni nzuri kwa sababu walionekana wana nia lakini hazitoshi. Pendekezo langu ni kuwa tuongeze ziwe shilingi bilioni tano ndiposa kaunti 11 ndogo zote zipate kadiri ya bilioni sita kila moja. Hilo litaonesha nia nzuri upande wa Kamati. Tunawauliza wasonge tu kidogo ifikie bilioni tano ili kaunti hizo ziridhike. Haya ni kwa sababu hata hizo kaunti zina majukumu mengi Ukitembelea Laikipia, hospitali zetu hazina dawa, barabara hakuna na shida ni nyingi. Kaunti ile ni kubwa sana na majukumu ambayo gavana anapaswa kutekeleza hayatoshelezwi i na hela zilizopendekezwa. Ndiposa kila mtu katika gatuzi anasema kwamba anangoja Rais aje afanye miradi. Wanatutuma kwa Rais ili aende akafanya ilhali gavana yuko pale. Ni kwa sababu hela nyingi zimebaki katika Serikali kuu. Ni jukumu letu kama Seneti kusema kuwa hela zinapaswa kufuata majukumu. Mfano ukulima umegatuliwa. Mambo ya masoko yamegatuliwa lakini majukumu hayo yanatekelezwa na Serikali ya Kitaifa. Hayo ni mambo tunayopaswa kuangalia hapa. Bi. Spika wa Muda, ninapendekeza rekebisho moja. Badala ya shilingi bilioni mbili ya usawazishaji kwa kuinua kaunti zilizo chini ninapendekeza kuongezwe ziwe shilingi bilioni tano na hilo linawezekana. Tusiseme tu hayo. Tueleze kinagaubaga kwa sababu kiwango kilichopendekezwa ni Kshs405 bilioni. Tunapaswa kusukuma zaidi kwa"
}