GET /api/v0.1/hansard/entries/1570379/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570379,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570379/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "sababu Seneti ilipitisha kuwa tunataka shilingi billion 465 na hiyo inawezekana tukifanya pamoja. Seneti iliyopita tulitembea pamoja na tukawa na kauli mbiu kuwa hakuna kaunti inayopaswa kupoteza hela. Bi. Spika wa Muda, nataka kuongea na Sen. Mungatana. Tulipofanya hivyo Seneti iliongeza ugavi wa pesa kwa shilingi bilioni 50. Hata sasa tuna uwezo tukitembea pamoja na tukiwa na nia kwa sababu umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Ninawaomba Maseneta wenzangu, tusiseme kuhusu shilingi bilioni nne na tano. Tulenge shilingi bilioni 465 kwa sababu, hili ndilo jukumu letu kubwa katika Seneti hii, kutetea gatuzi. Bi. Spika wa Muda, siku ya leo, Mswada tunaojadili leo ni mwafaka. Huu Mswada ndio umetuleta Seneti hii. Haijali mambo mengine yeyote. Hayo mambo mengine yawe kando kwa sababu, maneno tunayoongea kuhusu makaunti, vile kutafanyika na kutekelezwa, kutatekelezwa kulingana na hela ambazo siku ya leo tunatetea hapa. Hakuna mambo mengine tunapaswa kufanya kwa sababu, leo tunafaa kuongea kuhusu hizi hela na tukipata zile hela tunazozitaka, ziende kule gatuzi. Kuna mambo ya ufisadi na kuvuja kwa hela na hayo yatafwatiliwa na Kamati husika iliyowajibika vilivyo. Lakini, sisi tunafaa kutetea pesa ziende kwa kaunti. Hatuwezi tukasema kuna ufujaji wa hela na ufisadi kwa kaunti zetu, kwa hivyo, hatutatetea pesa. Si gatuzi zote zinafuja pesa. Kuna gatuzi zinafanya kazi vizuri, walio waeredi na stadi kwa kazi waliochaguliwa kufanya. Bi. Spika wa Muda, nitakwamwa hapa nikiwarai Maseneta wenzangu, haswa, Seneta wa Tana River pamoja na Seneta Mandago, wakubali hii jedwali, mahali pa udhibitisho ili tusawazishe kaunti hizi, tupewe bilioni tano. Ndio Seneta Mungatana akitembea Laikipia, apate barabara. Ukitembelea zahanati zetu, upate dawa. Sitaki kumwambia Seneta Mandago kwa sababu, yeye ni mwenzetu n ani jirani pia. Yeye siwezi kumhubiria, tayari ameokoka. Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Pia, ninaunga mkono ikiwa marekebisho ya bilioni tano katika jedwali hii yatafanywa."
}