GET /api/v0.1/hansard/entries/1570575/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1570575,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570575/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Mheshimiwa Spika, sijaridhika, kwa sababu nilitaka wachunguze kwa kina kama mjenzi wa jengo hili alitumia njia sawa. Kwa nini ameongezea gorofa zaidi zilizoshinda msingi na hivyo kusababisha Yusuf kupoteza maisha yake? Yusuf alikuwa ni mwanabiashara mdogo tu pale Marikiti. Ameacha mjane na watoto. Kufikia sasa, hatujui familia yake inakula nini. Bado tunaambiwa tu uchunguzi unaendelea, na imechukua muda mrefu sana. Naomba Wizara husika kuniambia kama mjane wa Yusuf na familia yake imefidiwa au la? Yusuf ashazikwa, lakini familia yake yahitaji kula na kusoma. Pia tunafaa kujua ni hatua gani imechukuliwa kwa mjenzi wa jengo hili badala ya gorofa sita akapeleka hadi 11. Asante sana."
}